Watendaji Mahakama ya VUGA matatani kwa tuhuma za rushwa.

Mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu uchumi zanzibar ZAECA imewakamata  watendaji wawili  wa Mahakama ya Vuga kwa  tuhuma za kupokea  rushwa  ya mirathi  ya familia ya watoto wa  tano.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Afisa Uhusiano Mamlaka ya rushwa Zanzibar Mwanaidi Sleiman Ali amesema watendaji hao akiwemo Mshika fedha  wa Mahakama ya Vuga pamoja na Mkaguzi  wa ndani wa mahakama hiyo wanatuhumiwa kufanya  kitendo hicho  ambacho ni kinyume na sheria hivyo hatua kali dhidi yao itachukuliwa kwa kufikishwa mahakamani.

Hata hivyo amesema upelelezi wa kesi hiyo   umekemilika  na  jalada la kesi la watuhumiwa hao linatarajiwa kufikishwa kwa mkurugenzi wa mashtaka DDP Jumatatu kwa lengo la kufungua kesi.

Aidha Afisa huyo amesema Marehemu  Rajab Khamis Hafidhi ambae ni baba wa watoto hao kabla ya kufariki kwake  aliwacha fedha Shilingi Milion 17  katika akaunt yake ya benki  ambapo   katika harakati za kugawana fedha hizo kwa watoto hao  watendaji hao  ndipo walipotaka kuwadhulumu.

Amesema  vitendo vya ubadhirifu wa mali za umma katika  taasisi za serikali bado vinaendela kujitokeza  licha ya mamlaka  kujitahidi kutoa elimu kwa  jamii kuwachana na tabia hizo lakini imeonekana kuwa   baadhi ya watendaji  wanayatumia  vibaya madaraka yao.

Mamlaka  imetoa wito kwa jamii  kuacha kujihusisha  na vitendo vya rushwa kwa kupokea au kutoa kwani sheria  haita mvumilia mtu  anapogundulika katenda  kosa.

chanzo;Zanzibar24

Comments