Mnyele, ambaye alikuwa wakili maarufu nchini kabla ya kuteuliwa kuwa
mkuu wa wilaya, imeelezwa kuwa ameamua kujiuzulu kwa sababu binafsi.
Lakini, akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, Mnyele alisema
kwamba, “Ukiteuliwa, mamlaka husika inatoa taarifa, na ukiondoka katika
nafasi hiyo mamlaka inatoa taarifa. Kwa hiyo mtafuteni Msigwa
(Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu). Lakini sisi tuko huku
tunaendelea na kazi.”
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri hakupatikana kuelezea kwa
undani uamuzi huo, lakini gazeti hili limethibitishiwa na viongozi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Uyui kwamba Mnyele amejiuzulu na aliwaeleza
hayo jana alipopita kuwaaga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Said Ntahondi alisema
kwamba anawatakia kila la heri katika majukumu yao ya kazi. Alisema
kwamba licha ya yeye (DC Mnyele) kuondoka, anatambua kuwa mapambano juu
ya maendeleo ya Uyui, yataimarika kwa watumishi wote wa halmashauri
hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa yao, Mnyele alipita kila Idara za Halmashauri ya Wilaya hiyo kuaga akianzia na watumishi wa ofisi yake.
Taarifa za awali zinasema kuachia kwake ngazi ya ukuu wa wilaya
imetokana na kutingwa na majukumu mengi binafsi aliyonayo, na kwamba
imedaiwa kuwa mkuu huyo wa wilaya aliandika barua mwaka jana akiomba
kujiuzulu nafasi hiyo, kwani ametingwa na majukumu mengine binafsi.
Taarifa zaidi zinasema baada ya kuandika barua ya kuutema ukuu wa
wilaya, barua yake imejibiwa na amekubaliwa kuachia nafasi hiyo.
Mnyele alikuwa mmoja wa wakuu wa wilaya 139 walioteuliwa na Rais John
Magufuli, Juni 26, 2016, ambao ilielezwa kuwa amezingatia mambo kadhaa,
ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya
miaka 60 ameamua wastaafu.
chanzohabarileo.
Comments