Wachimbaji wa madini 15 waliokuwa wamefukiwa kwenye mgodi wa RZ mkoani Geita waokolewa wakiwa hai.

Watu 15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi Geita wakati wakiwa kazini katika moja ya migodi mkoani humo waokolewa wakiwa hai.

Zoezi la kuwaokoa wachimbaji wa madini 15 walionasa kwenye mgodi  wa RZ Union uliopo mkoani Geita limemalizika kwa wachimbaji wote hao kuokolewa wakiwa hai  Taarifa kutoka eneo la tukio zime sema kuwa zoezi hilo lilifanikiwa baada ya mbinu za uokoaji kuboreshwa na watu hao waliokolewa wamepewa huduma ya kwanza baada ya kuokolewa na sasa wamepelekwa hospitali kwa uangalizi zaidi.

Leo ilikuwa ni siku ya nne tangu wachimbaji hao wa madini wanase katika mgodi huo ambapo mmoja kati watu ambao  walikuwepo siku zote kusimamia zoezi hilo la ukoaji alikuwa ni mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga.

chanzo; zanzibar24.

Comments