Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hati za kuunganisha vyuo vitatu vya Zanzibar huko katika Chuo kikuu cha taifa Suza Waziri Riziki amesema wasomi wa vyuo vikuu ni miongoni mwa watu wanaochangia katika kuengeza pato la serikali hivyo si vyema kwa viongozi waliopo kushindwa kutunza rasilimali hizo.
Aidha amesema muungano wa vyuo hivyo utahautaathiri shughuli za masomo yanayofundisha kwa wananfunzi badala yake utasaidia kuinua kiwango cha elimu Nchini na kutowa wito kwa walimu na wanafunzi kuzidisha ushirikiano ili kufikia lengo la Zanzibar kuwa na taifa la wasomi.
Kwa upande wake Baada ya kukabidhi hati za Chuo cha Utalii Zanzibar Waziri wa Habari, Utalii Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma amesema kutokana na Zanzibar kutegemea kwa kiasi kikubwa sekta ya utalii muungano wa vyuo hivyo utaimarisha uzalishaji wa wataalamu wa fani hiyo watakao saidia kukuza pato la taifa.
Jumala ya vyuo vitatu vimeunganishwa pamoja katika Chuo kikuuu cha Taifa SUZA ikiwemo Chuo cha Fedha Chwaka ,Chuo cha Utalii Maruhubi na Chuo cha Afya Mbweni ili kujenga msingi imara wa Elimu inayotolewa na Vyuo vikuu Zanzibar.
chanzo:Zanzibar24
Comments