Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven ametoa amri ya kukamatwa viongozi hao wakati yeye na wao wakiwa mkutanoni.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya ametekeleza amri hiyo, watuhumiwa wamekamatwa muda huo huo.
Zelothe amewaagiza wakuu wa wilaya mkoani humo kuhakikisha watumishi
wote wa umma waliosababisha matumizi mabaya ya fedha hizo kwa kuwaingiza
wasiostahiki katika mpango huo, zikiwemo kaya hewa, wanakamatwa na
kufikishwa mahakamani.
Baada ya kusikiliza kero za wanufaika wa mpango huo, Zelothe
alimwagiza Mkuu wa Polisi wilayani hapa kuwakamata viongozi hao tisa wa
serikali ya kijiji cha Serengoma, wanaotuhumiwa kujinufaisha na fedha
hizo.
Zelothe amempa Mkuu wa Wilaya siku moja ahakikishe watuhumiwa wote 50 wamekamatwa na washitakiwe mahakamani.
Amewataka wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za wilaya za Kalambo,
Nkasi, Sumbawanga na Manispaa ya Sumbawanga wahakikishe wanataalamu wao
wanawasaidia wanufaika wa mpango huo ili watumie fedha wanazopata kwa
manufaa.
"Serikali haitasita kuwachukulia hatua watakaonda kinyume na utaratibu,” alisisitiza.
Imeelezwa kuwa kaya 866 zikiwemo kaya hewa 195 zimeondolewa katika
mpango huo mikoani Rukwa na Katavi wakati wa uhakiki uliofanyika kuanzia
Februari hadi Oktoba mwaka jana.
chanzo;habarileo.
Comments