Pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa, Henry Msunga wengine ni Katibu
UVCCM, Salum Kidima na Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, Egla
Mwamoto. Wametaka kusimamishwa huko kuambatane na uchunguzi wa tuhuma
zinazowakabili viongozi hao katika fedha na matumizi ya mamlaka.
Wakizungumza na waandishi wa habari mjini hapa ikiwa ni siku moja
mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kikanuni cha baraza la vijana
mkoa wa Dodoma , Mwenyekiti wa UVCCM Chamwino, Fransis Gombo, alisema
wamefikia uamuzi wa kutoa ombi hilo kupitia vyombo vya habari baada ya
kuona hoja zao hazifanyiwi kazi huku jumuiya hiyo mkoani ikizidi
kudidimia.
Akiwa na wajumbe wengine katika mkutano huo Gombo alisema tangu mwaka
2014 viongozi hao hawajaitisha kikao chochote cha kikanuni. Gombo
alisema kumekuwepo na matumizi mabaya ya fedha za jumuiya ikiwamo sehemu
ya maandalizi ya harusi ya mwenyekiti.
Aidha alisema kuna mradi wa vibanda zaidi ya 100 vilivyopo katika
ndani ya eneo la soko la Sabasaba ambavyo vinamilikiwa na UVCCM mkoa wa
Dodoma, lakini umeonekana kama hauna mwenyewehuku anayekusanya fedha
akiwa hajulikani.
Imedaiwa kwa waandishi wa habari na Gombo kwamba wapangaji wa vibanda
hivyo hulipa kiasi cha laki moja na nusu mpaka laki mbili, lakini
viongozi wao wamekuwa wakiwapa taarifa wajumbe kuwa wapangaji wanalipa
kodi kati ya Sh. elfu kumi mpaka elfu ishirini.
Aidha msemaji huyo amesema kwamba kuna haja kwa uongozi wa Chama
kumuondoa Kaimu Katibu wa CCM Mkoa, Jamila Yusufu, kwa madai kuwa hawana
imani naye na amepoteza sifa ya kuwa mlezi wa jumuiya hiyo.
Pia wamemtuhumu katibu huyo, kwa kuvuruga kikao cha baraza
kilichofanyika juzi, Januari 19 mwaka huu kwa kuegamia upande mmoja na
kumuondoa mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Dodoma ndani ya kikao kabla kikao
hicho hakijamalizika.
Akizungumzia tuhuma hizo Mwenyekiti wa UVCCM mkoa Msunga, alikanusha
kuhusika na tuhuma zozote huku akisema kuna utaratibu wa kushughulika na
tuhuma za ubadhirifu ndani ya chama unaohofiwa ama unaofanywa na
viongozi.
Mwenyekiti huyo, alisema, kuhusiana na tuhuma za fedha za jumuiya
kutumika katika harusi yake hana taarifa na jambo hilo, labda kama
atapewa taarifa kuwa kuna fedha zilitolewa na kutumika, lakini binafsi
hajui chochote anachofahamu ni kwamba harusi yake aliigharamia mwenyewe
na ilikuwa ya gharama kubwa.
Kuhusu vibanda vya sabasaba alisema, kodi inayotozwa ni Sh10,000 kwa
kibanda kimoja ambapo baadaye iliongezwa kufikia Sh20,000 ambayo ndiyo
inayotozwa mpaka sasa.
Pia alisema kikao cha baraza cha Januari 19 mwaka huu kiliahirishwa
mpaka Januari 26, mwaka huu, kutokana na baadhi ya mambo kutokamilika.
Naye Kaimu Katibu wa CCM mkoa, Jamila, alipohojiwa kuhusiana sakata
hilo, alisema, Chama kina utaratibu wake mambo ya chama sio ya
kuzungumza kwenye vyombo vya habari, huku akidai kuwa fukuto hilo la
umoja wa vijana mkoa wa Dodoma, huku akigoma kuendelea kutoa ufafanuzi
zaidi kwa madai kuwa yuko katika maandalizi ya uchaguzi wa Udiwani Kata
ya Ng’ambi.
Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa, Egla, alipohojiwa kuhusiana na
maazimio hayo, alitaka kujua ni kikao kipi kilichoazimia maazimio hayo
kwa kuwa yeye anachofahamu ni kwamba kikao kilichokaa Januari 19
kiliahirishwa na kitafanyika tena Januari 26 mwaka huu.
chanzo;habarileo.
Comments