Msemaji wa Antonio Guterres amesema hatua ya upande
mmoja inaweza kuwa ni kikwazo cha kuelekea amani ya ufumbuzi wa tatizo
hilo kwa kuwepo kwa mataifa mawili.
Umoja wa Mataifa unauzingatia ujenzi huo wa makaazi kama siyo halali.
Uamuzi
huo ulisisitizwa tena mwezi uliopita katika azimio la Baraza la Usalama
ambapo utawala wa Rais aliyemaliza muda wake nchini Marekani Barack
Obama uliukataa kwa kupiga kura ya VETO.
Hata hivyo, Waziri mkuu
Benjamin Netanyahu na waziri wa ulinzi Avigdor Lieberman wamesema
wanakubaliana na hatua hiyo, kutokana na mahitaji ya nyumba
yaliyokuwepo.
Kwa upande wa maafisa wa Palestina wanasema
mipango hiyo inaondoa matumaini ya kuwepo kwa amani, kutokana na Israel
kujenga makaazi yake katika ardhi wanayoitaka kuwa taifa lao la baadaye.
Wasel
Abu Yousef mwanachama mwandamizi wa chama cha Wapalestina PLO anataka
hatua za kimataifa kuchukuliwa juu ya uamuzi huo wa Israel.
Mwandishi
wa BBC mjini Jerusalem amesema serikali ya Israel ni wazi inahisi
kutiwa hamasa na Donald Trump, ambaye aliahidi kuwa upande wa Israel
zaidi ya mtangulizi wake.
chanzo:bbc
Comments