Muda mfupi baada ya kukagua gwaride la kuapishwa
kwake, Bwana Trump, alitia amri ya serikali, kupunguza mzigo wa kiuchumi
kwa taifa, unaotokana na gharama za kufadhili bima ya matibabu ya bei
nafuu inayofahamika kama Obama Care, ambayo Trump aliahidi kufanyia
marekebisho.
Trump pia ametia saini amri ya kuwaidhinisha mawaziri wake wapya wa
Ulinzi na usalama wa kitaifa ambao uteuzi wao umepitishwa na bunge la
seneti.
Utawala wa Trump pia umeaanza kufanyia marekebisho mtandao
wa kijamii wa Ikulu ya White House kwa kuweka masuala yatakayopatiwa
kipaumbele na uongozi huo mpya.
chanzo;bbc
Comments