Shirika
hilo linamtuhumu kiongozi huyo kwa kikiuka marufuku iliyowekwa kwenye
katiba dhidi ya kupokea malipo kutoka kwa serikali za nchi za nje.
Kundi
la mawakili na watafiti linasema Bw Trump amekuwa akipokea malipo
kutoka kwa serikali za nje kupitia wageni kwenye hoteli zake na majumba
yake ya kukodisha.
Wanasema kuna kifungu kwenye sheria ya nchi hiyo ambacho kinaharamisha malipo kama hayo.
Mwanawe Donald Trump, Eric, ametaja hatua hiyo kama "usumbufu tu kwa nia ya kufaidi kisiasa".
Eric Trump, ambaye ni makamu rais mtendaji wa shirika la Trump
Organization ambalo linamiliki na kusimamia biashara za rais huyo,
amesema kampuni hiyo imechukua hatua kubwa kufuata sheria kuzuia kesi,
kwa mujibu wa New York Times.
Amesema kampuni hiyo imeahidi kutoa
faida kutoka kwa hoteli zake ambazo zimetokana na wageni kutoka serikali
za nje na kuziwasilisha kwa Hazina Kuu ya Marekani.
Shirika
hilo la Citizens for Responsibility and Ethics in Washington (Crew)
limesema litawasilisha kesi katika mahakama ya Manhattan, New York
Jumatatu asubuhi.
"Hatukutaka kufika hapa," mkurugenzi mkuu mtendaji Noah Bookbinder alisema kupitia taarifa.
"Matumaini
yetu yalikuwa kwamba Rais Trump angechukua hatua zifaazo kuzuia kukiuka
Katiba kabla yake kuingia madarakani. Tumelazimishwa kuchukua hatua za
kisheria."
Katiba ya Marekani inasema hakuna afisa yeyote wa serikali anayefaa
kupokea zawadi au "malipo yoyoye ya kifedha, au ada kutoka kwa serikali
ya kigeni.
Mawakili wa Bw Trump wanadai sheria hiyo ni ya kutumiwa
tu kuzuia maafisa wa serikali kupokea zawadi au manufaa maalum kutoka
kwa nchi za nje na wala si kwa malipo kama vile bili ya hoteli.
chanzo:bbc.
Comments