Mradi huo ulikuwa unafanyika kwa msaada wa serikali ya Ujerumani.
Mkuu wa Mkoa Kigoma, Emmanuel Maganga, akitoa taarifa ya utekelezaji
wa shughuli mbalimbali za maendeleo kwa mwaka 2016 amesema kuwa mradi
huo ulipaswa kukamilika Machi mwaka huu na kwa hatua hiyo mradi huo
hautaweza kukamilika kama ilivyokusudiwa.
Alisema kwa muda sasa mkandarasi huyo ameshindwa kuingiza pesa za
kuendelea na hatua za utekelezaji wa mradi baada ya pesa alizokuwa
akilipwa na kuingizwa kwenye akaunti yake kuchukuliwa na taasisi
zinazoidai kampuni hiyo.
Pamoja na hatua ya kuvunja mkataba huo, serikali pia imezuia mali na mitambo yote ya kampuni hiyo.
Amewataka wananchi kuzuia mitambo katika maeneo ya miradi isiondolewe kwa namna yeyote.
Akielezea hali hiyo, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Kigoma, Aziz
Mutabuzi alisema kufuatia kufilisika kwa kampuni hiyo, Wizara ya Maji na
Umwagiliaji imeanza kuchukua hatua kuona namna ya kutafuta mkandarasi
wa kuukamilisha mradi huo.
Pia serikali inatarajia kununua pampu mpya kuongeza uwezo wa
uzalishaji maji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Kigoma/ Ujiji wakati
taratibu nyingine zikiendelea.
Alisema ili kukamilisha mradi huo, kiasi cha sh bilioni 32
zinatarajiwa kutumika. Kwa sasa, mradi umetekelezwa chini ya asilimia
50.
chanzo;habarileo.
Comments