Mratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania
(TAMWA) Dk. Mzuri Issa Ali amesema wanawake wa kijijini wengi wao
masikini wamehamasika kujikwamua kiuchumi lakini wanakwamishwa na suala
la umiliki wa ardhi.
Amesema jumla ya maombi 101 ya usajili wa ardhi katika mkoa wa Kusini
Unguja yamefikishwa katika Mamlaka mbali mbali ikiwemo kwa Sheha katika
hatua ya awali lakini yanalalamikiwa kutokana na gharama kubwa.
Hivyo ameiomba serikali ipitie sera na utaratibu wa ardhi katika
mwaka huu mpya ili kuleta usawa wa kijinsia kwa kuwapunguzia wanawake
gharama za usajili wa ardhi.
Amesema gharama za usajili wa ardhi wa zaidi ya shilingi laki 2
kuanzia kwa Sheha, Wilaya na Kamisheni kunafanya usajili huo kukwama
katika hatua ya mwanzo na mwisho.
Nae Mwenyekiti wa mtandao wa ardhi wa Wilaya ya Kati Bahati Issa
Suleiman amesema mwaka uliopita jumla ya wanawake 107 wamejitokeza
kuomba fomu ya umiliki wa ardhi na kati yao sita ndiyo waliofanikiwa.
chanzo;Zanzibar24
Comments