Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake
kwenye majumuisho ya ziara yake katika masoko makuu ya mjini Musoma
kujionea hali ya bei na upatikanaji wa chakula kwa wakazi wa mkoa wa
Mara wanaokadiriwa kufikia milioni 1.7.
Alisema mkoa huo una ziada ya tani 461,000 za nafaka zilizovunwa
Julai katika msimu wa mwaka jana, chakula ambacho kinaufanya
ujihakikishie hali ya usalama wa chakula hadi Mei mwaka huu.
“Hata hivyo, msimu wa mvua za vuli haukutuacha bure kwani tumeendelea
kujikusanyia tani nyingine zaidi ya 200,000 za nafaka ambazo
zinauhakikishia mkoa kubaki salama kwa chakula hadi Agosti,” alisema.
Alikiri kuwepo kwa ongezeko la bei kwa baadhi ya vyakula
vinavyotumiwa kwa wingi na wenyeji na kusema kuwa, hali hiyo
itarekebishwa vyakula vitakapoongezeka kwenye masoko.
Dk Mlingwa aliwataka wananchi kuendelea kutumia ziada hiyo ya chakula kwa uangalifu ikiwa ni pamoja na kutotengenezea pombe.
Pia, aliwataka kufanya maadalizi ya kilimo kwakuwa msimu wa masika umekaribia.
chanzo;habarileo.
Comments