Nana Akufo-Addo, aliyekuwa
wakati mmoja wakili wa haki za kibinadamu, alimshinda kiongozi wa sasa,
John Dramani Mahama, katika uchaguzi wa mwezi uliopita.
Karibu viongozi 11 wa mataifa ya Afrika wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo, ambako hali ya usalama tayari imeimarishwa.
Baada
ya kuapishwa kwake, viongozi wa Afrika watajadiliana jinsi ya
kuhakikisha kuwa Rais wa Gambia Yahya Jamme anakubali kuwa alishindwa
katika Uchaguzi Mkuu uliopita.
chanzo:bbc.
Comments