Akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Bariadi mkoani Simiyu
Rais Magufuli amesema kuwa taarifa hizo ni uzushi huku akisema kuwa kama
yeye Rais wa Tanzania yeye ndiye mwenye mamlaka ya kutoa taarifa za
njaa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.
“Wapo wafanyabiashara wengine wachache waliokuwa wamezoea panapotokea
matatizo kidogo tu ya ukame wanatumia vyombo vya habari ikiwa pamoja na
magazeti wanayoyaamini wao sio magazeti yote, pamoja na baadhi ya
wanasiasa kuzungumza Tanzania kuna njaa, anayejua njaa ni Rais na sio
gazeti fulani mimi ndiyo niliyepewa dhamana ya kuwaongoza Watanzania,”
alisema.
Hivi karibuni kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akiwa
katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani wa Kata ya Nkome
mkoani Geita aliitaka serikali kutangaza balaa la njaa.
chanzo;zanzibar24.
Comments