Polisi yapiga marufuku matembezi ya jumuiya ya vijana ya chama cha CUF.

alawitiJeshi la polisi Zanzibar limepiga marufuku matembezi ya amani yaliyokusudiwa kufanywa na Jumuiya ya vijana wa Chama cha Wananchi CUF Wilaya ya mjini yenye lengo la kuwakumbuka Watanzania waliokufa Siku ya tarehe 26/27 ya mwaka 2011.

Akizungumza na waandishi wa Habari huko ofisini kwake madema kamanda wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Nassir  amesema maandamano hayo sio ya halali kufanyika na kuwataka vijana wa CUF kuacha kufanya maandamano hayo ambayo hayatambuliki kisheria.

Aidha amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi halitasita kuwachukulia hatua za kisheria kwa watu watakaojihusisha na matembezi  hayo yaliyolenga kuazia Muembe tanga  na kumalizikia Kinazini Mjini Zanzibar kutowa wito kwa jamii kuendelea na shughuli zao za kijamii.

chanzo: Zanzibar24.

Comments