Mbali ya hilo, vikosi hivyo vya ulinzi vilifanikiwa kuteketeza ekari
31 za mashamba ya bangi zoezi zima lilifanyika kwa siku mbili katika
wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa polisi nchini ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Kupambana na Kudhibiti
Dawa za Kulevya, Mihayo Msikhela alisema kuwa operesheni hiyo ilifanyika
majira ya saa 11 alfajiri, Januari 10 hadi 12 katika wilaya ya Arumeru,
kijiji cha Kisimiri Juu na kufanikiwa kuteketeza mazao hayo haramu.
Msikhela alisema operesheni hiyo ni ya nchi zima lakini wameanzia
katika Mkoa wa Arusha, wilaya ya Arumeru wenye sifa kubwa ya kilimo cha
bangi hapa nchini.
Alisema wilaya zinazoongoza kwa kilimo cha bangi hapa nchini ni
Arumeru na Tarime na kusema kuwa watu wanaofanya biashara hiyo wanaombwa
kuacha mara moja vinginevyo vyombo vya dola havitasita kuwachukulia
hatua kwa kulima kilimo cha bangi.
Msikhela aliwaasa viongozi wa serikali ngazi ya kijiji na kata
kuwafichua wanaofanya shughuli hiyo kwani wao ndio wanaowajuwa lakini
wanawaficha kwa maslahi yao hivyo nao watachukuliwa hatua kali.
“Tunataka viongozi wa serikali wa ngazi hizo kushirikiana na polisi
kuwafichuwa wahusika bila ya woga lakini hilo halifanyiki…kuna taarifa
kuwa viongozi wanashiriki kuwahifadhi wakulima wa kilimo cha bangi, nao
tutawatia mbaroni kwa kuwa nao ni wahalifu kwa kuficha wahalifu,”
alisema.
chanzo;mpekuziblog.
Comments