Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekishauri Chama cha ACT – Wazalendo na
Vyama vingine vyenye wagombea wa Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo
la Dimani na Udiwani katika Kata Ishirini (20) za Tanzania Bara
,kuwasilisha malalamiko ya ukiukwaji wa Maadili ya Uchaguzi kwenye
Kamati za Maadili zilizo katika maeneo yao.
Akizungumza na vyombo vya habari jana jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhan alisema
NEC imepata taarifa kupitia Vyombo mbalimbali juu ya malalamiko ya
Chama Cha ACT-Wazalendo kuvilalamikia Vyombo vya Dola pamoja na
Watendaji wa Umma kufanya vitendo vyenye muelekeo wa kukipendelea Chama
Cha Mapinduzi (CCM).
Bw. Kailima alisema
taarifa ya Chama hicho iliyotolewa kwenye Vyombo vya Habari Januari, 12
2017, imeeleza kuwa Watendaji wa Halmashauri ya Geita waliwakusanya
Wazee katika Kata ya Nkoma waje na Vitambulisho vyao vya kupigia Kura
kwa lengo la kuwapatia huduma ya afya bure jambo linalolalamikiwa na
ACT- Wazalendo kwa madai kwamba Watendaji hao wana lengo la kuwahadaa
Wazee hao ili wakipigie Kura Chama Cha Mapinduzi (CCM).
chanzo;mpekziublog.
Comments