Katika taarifa yao ya pamoja walioitoa katika mkutano
uliofanyika katika mji mkuu wa Niger, Niamey, viongozi hao kutoka nchi
za Burkina Faso, Mali na Niger wamesema eneo hilo kwa haraka linakuwa
kimbilio kwa makundi ya kila aina ya ugaidi.
Mwenyeji wa mkutano
huo Rais Mahamadou Issoufou amesema jeshi la pamoja la ulinzi litafanya
kazi sawa na operesheni za pamoja zinazofanywa na majeshi ya Nigeria,
Niger, Chad na Cameroon dhidi ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram,
katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Makundi ya
wapiganaji wa kiislamu yenye mafungamano na mtandao wa Al Qaeda, katika
siku za hivi karibuni yamefanya mashambulizi katika eneo hilo kwa
kupitia sehemu za jangwa.
chanzo:bbc.
Comments