Mwanamke akamatwa na mabunda 15 ya bangi Pemba.

jeshi la polisi mkoa wa kaskazini pemba limefanikiwa kumkamata mwanamke mmoja alijulikanwa kwa jina la Sakiri mohd khamis mwenye umri wa miaka 50 mkaazi wa mkamasini wilaya ya micheweni  mkoa wa kaskazini pemba na mabunda 15 ya majni makavu yanayosadikiwa kuwa ni bangi.

Akithibitisha kukamatwa kwa mwanamke huyo  kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini Pemba Haji Khamis  amesema ukamatwaji wake  wake ni kutokana na taarifa za awali kuwa mwanamke huyo kuwa anayo tabia ya kuuza bangi.

kufuatia taarifa hizo ndipo jeshi la polisi liliamua kufanya upekuzi ndani ya nyumba yake  na kukamata mabunda 15 ya majanin makavu na kila moja likiwa  na gram 500  kwa sasa mwanamke huyo anashikiliwa najeshi la polisi  na hatua za kupelekwa mahakamani  unafanywa.

 chanzo;zanzibar24

Comments