Mwalimu mkuu na msaidizi wake wasimamishwa kazi kwa kuwatoza wazazi shilingi 10000.

Related imageMkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba, amewasimamisha kazi mwalimu mkuu wa skuli ya mitiulaya na msaidizi wake kutokana na kitendo cha kuwatoza fedha ya shilingi 10000 wazazi wanoandikisha watoto wao katika muhula mpya wa masoma katika skuli hiyo.
Waliosimamiswa kazi ni Abdallah ali Mohd na Husna Salim Suleiman ambae ni msaidizi wake.
Amesema wamelazimika kuchukua uamuzi huo ili kulinda hadhi ya serikali pamoja na uamuzi wa Rais ambae aliwathibitishia wananchikuwa hakuna mzazi ataetoa pesa ili mtoto wake apate nafasi ya kuanza masomo.
Aidha alisema Serikali ina nia thabiti ya kusimamia na kutekeleza majukumu yake kikamilifu ili kuleta maendeleo kwa wananchi  wao.
Kwa upande wake Ofisa elimu na mafunzo ya amali mkoa wa kaskazini Pemba, Mohd Nassor Salim  alisema uamuzi uliochukuliwa na Serikali ya Mkoa ni mzuri kutokana na walimu hao kukiuka misingi ya utumishi.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na muandishi wa habari hizi wameipongeza serikali ya mkoa kwa uamuzi huo kwani hali hiyo ya kutozwa pesa iliwawia vigumu hususan kwa wazazi wenye mtoto zaidi ya mmoja.
Adhabu ya kusimamiswa kazi walimu hao itaendelea hadi pale wizara ya elimu na mafunzo ya amali itakapochukua hatua kwa mujibu washeria na taratibu za utumishi wa umma juu ya kiendo hicho.
chanzo;zanzibar24.

Comments