Jenerali Kainerugaba amekuwa kamanda wa kikosi maalum cha wanajeshi
(SFC) chenye jukumu la kutekeleza operesheni maalum za kijeshi.
Kikosi hicho husimamia ulinzi wa rais na kulinda maeneo muhimu kwa serikali Uganda.
Luteni kanali Don Nabaasa amepandishwa cheo na kuwa kanali na akateuliwa kaimu kamanda wa SFC.
Rais Museveni pia amemteua mkuu mpya wa majeshi, Meja Jenerali David Muhoozi ambaye amepandishwa cheo na kuwa jenerali.
Mkuu wa majeshi wa awali, Jenerali Edward Katumba Wamala amehamishwa na kuteuliwa waziri wa ujenzi.
Kwenye mabadiliko hayo yaliyotangazwa na msemaji wa Majeshi ya Ulinzi
ya Uganda (UPDF) Luteni Kanali, Rais Museveni amempandisha afisa mkuu
wa majeshi aliyeongoza operesheni ya kushambulia ikulu ya mfalme wa
Rwenzururu, magharibi mwa nchi hiyo.
Watu 100 walifariki wakati wa operesheni hiyo. Mfalme wa Rwenzururu Charles Wesley Mumbere alikamatwa na bado anazuiliwa.
Brigidia
Peter Elwelu, aliyekuwa mkuu wa kikosi cha wanajeshi hao wenye kambi
yao kuu Mbarara, amepandishwa cheo na kuwa meja jenerali na akateuliwa
kamanda wa majeshi ya nchi kavu.
chanzo;bbc
Comments