
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 12:45 maghribi mara baada ya mama mzazi wa mtoto huyo Fatma Hafidh alipokua akisali na baada ya kumaliza na kutoka nje ndipo alipomuona mtoto wake akiwa katika ndoo hiyo.
Akizungumza kwa majonzi baba mzazi wa mototo
huyo Saidi Mbarouk amesema kua mara baada ya kutokea tukio hilo
waliamua kumchukua mtoto na kumkimbiza katika hospitali ya Abdallah Mzee
na ndipo walipopatiwa majibu kua ameshafariki dunia.
“kama
tunavyojua sote ni wa mungu na hakika sote tutarejea kwake hii ni
asababu tu na kila mmoja na wakati wake na ukifika hakuna ujanja
tunamshukuru mungu kwa tukio hili” alisema bw Hafidh.
Amesema
kutokana na mkasa huo hawanabudi kumshukuru Mwenyezimungu kwakua kifo
ni haki ya kila mtu na kilichotokezea ni sababu tu ya kifo chake.
Babu
wa mtoto Bw Kassim Juma Abdallah amemuambia mwandishi wa habari hizi
huku akionekana kua na simanzi kua ingawa wanaumia sana kutokana na
tukio hilo lakini bado wamo katika subra wakiamini kua hiyo ni mipango
ya Allah SW.
Kwa
upande wake sheha wa shehia ya Mizingani Bw Rajab Mbwana Rajab amesema
kua amelipokea tukio hilo kwa mshituko mkubwa huku akisema kua ni la
kuhuzunisha hasa kwa wanafamilia hiyo kuondokewa na kipenzi chao.
Sheha huyo amewataka wafiwa kua na moyo wa subra kwani mauti ni haki ya kila mtu.
Sambamba
na hayo amewataka wazazi na walezi wa watoto kuzidisha umakini katika
malezi ya watoto kwa kujua mazingira wanayochezea watoto wao pamoja na
kuweka pembeni au mbali vitu vyote vile vitakavyokua na muonekano wa
kuweza kusababisha hatari kwa mtoto.
Kamanda
wa polisi mkoa wa kusini Pemba Shekhani Muhammed Shehan amesema kua
mpaka sasa hakuna taarifa ya tukio hilo iliyoripotiwa katika kituo cha
polsi.
Amesema inaonekana wanafamilia hiyo hawakutoa taarifa katika kituo cha polsi.
Habri
kutoka kwa wanafamilia ya mtoto huyo zinasema kua mtoto Khadija
alifariki tokea nyumbani na waliamua kumpeleka hospitali ili kwenda
kupata uthibitisho tu wa daktari.
Wananchi
kutokana maeneo mablimbali ya shehia ya Mizingani walikusanyika pamoja
leo saa 1 za asubuhi kuuzika mwili wa mtoto huyo huko
Kichinjuu,Innalalillahi wainnailyhirajiun.
chanzo;zanzibar24.
Comments