Abdulrazak Juma Seif mkaazi wa Darjabovu ameachiwa huru na Hakimu
Valentine Andrew Katema, baada ya upande wa mashtaka kushindwa
kuthibitisha kosa kwa mtuhumiwa huyo.
Mshtakiwa huyo alifikiswa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza April 16
2015 na kushitakiwa kwa kosa la kubaka msichana aliye chini ya
uangalizi wa wazazi wake.
Shitaka hilo ambalo alilikana lilisomwa chini ya vifungu vya 125(1)
(2) (e) na 126 (2) vya kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za
Zanzibar.
Tukio hilo lilidaiwa kutokea Januari 26/ 2015 majira ya saa 1:50
asubuhi ambapo mtuhumiwa alimbaka msichana huyo huko maeneo ya
darajabovu.
Upande wa mashitaka ulileta mashahidi wanne lakini hata hivyo
ushahidi huo haukuweza kushawishi Mahakama kama mshtakiwa huyo alihusika
kutenda kosa hilo.
Hivyo Hakimu Valentine aliamua kumuachia huru mtuhumiwa huyo kwa
mujibu wa sheria huku akitoa haki ya kukata rufaa mahakama kuu ya
Zanzibar kwa upande uliokua haujaridhika.
chanzo;zanzibar24.
Comments