Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameyaonya
magazeti mawili yanayoandika habari za uchochezi na kupotosha wananchi
kwa kuwa vinahatarisha amani ya nchini.
Ametoa onyo hilo jana wakati akikagua na kufungua Kiwanda cha Jambo cha kuzalisha vinywaji baridi mkoani Shinyanga.
Rais
Magufuli alisema Serikali haitayavumilia magazeti hayo mawili kwa
kuandika habari za uchochezi ambazo zinaweza kuhatarisha amani ya nchi
kama ilivyotokea katika nchini ya Rwanda na kupelekea mauaji ya kimbari
nchini humo.
chanzo;mpekuziblog.
Comments