Mmoja afariki kwa kuangukiwa na nyumba hurumzi.

Mtu Mmmoja amefariki dunia na Mwengine kujeruhiwa Baada ya kuangukiwa na Nyumba katika maeneo ya hurumzi wakati walipokuwa wakiendelea na shughuli za Ujenzi wa nyuma hiyo.

Akizungumza na waandishi wa Habari baada ya tukio hilo huko ofisini kwake Kamanda wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Nassir  amesema Tukio hilo limetokea majira ya saa sita na nusu mchana ambapo nyumba hiyo imeanguka na kusababisha kifo na majeruhi pamoja na kuharibu pikipiki moja ambayo iliegeshwa pembezoni mwa nyumba hiyo.

Aidha amesema alifariki dunia ni Khamis kombo Awesu miaka 35 mkaazi wa bubwini na majeruhu Mabrouk Vuai Seif miaka 40 mkaazi wa Bubwini ambaye anaendelea na matibabu katika hospitali kuu ya Mnazi mmoja.

Hata hivyo amesema pikipiki iliathirika na tukio hilo ni mali ya Hassan Nassor Mgeni yenye namba za usajili Z 320 BU.

Wakizungumza na Zanzibar 24 kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wa maeneo hayo wameziomba taasisi zinazohusika kusimamia nyumba hizo kuharakisha huduma za ukarabati wa majengo hayo ili kunusuru maisha ya watu wanaotumia maeneo hayo kwa shughuli zao za kijamii.

Hata hivyo wamesema kwa kipindi kirefu wanakua mstari wa mbele katika kutoa taarifa sehemu husika kabla ya maafa lakini viongozi wa taasisi zinazosimamia wanashindwa kutoa ufafanuzi kwa haraka.

Nyumba hiyo yenye namba 19/54 inayomilikiwa na kamisheni ya wakfu na mali ya amana aliyopangishwa Bw. Ali Nassor Muhammed mkaazi wa Mbuyuni.

chanzo; Zanzibar24.

Comments