Mkuu wa Mkoo wa Mrogoro Aagiza Kusakwa Wafugaji wavamizi.

Mkuu wa mkoa wa morogoro mh kebwe steven kebwe ameuagiza uongozi wa serikali wilayani mvomero kuhakikisha wanawasaka usiku na mchana wafugaji wavamizi wanaoingiza mifugo kinguvu katika mashamba ya wakulima na kuharibu mazao.

Mkuu wa mkoa ameyasema hayo katika ziara yake ya kutembelea vijiji vya maharaka na mlandizi vilivyoko katika wilaya hiyo ambavyo vimekumbwa kwa kiasi kikubwa na uvamizi huo.

Wakitoa masikitiko yao mbele ya mkuu wa mkoa wananchi hao wamedai wafugaji wamekuwa wakitumia nguvu ya pesa kuweza kuwalaghai baadhi ya viongozi na kuweza kuwaruhusu kuingiza mifugo na kuharibu mazao yao jambo ambalo limesabisha uharibifu mkubwa wa mazao na huenda likasababisha janga kubwa la njaa ,

Kufuatia malalamiko ya wananchi hao mh,mkuu wa mkoa amemuagiza mkuu wa wilaya hiyo muhamed utaly kuhakikisha wanawasaka na kuwaondoa wafugaji wote wavamizi waliofavia katika maeneo ya wakulima na watakaobainika hatua kali za kisheria zichukuliwe zidi yao ili iwe fundisho kwa wengine.

"mkuu wa wilaya na mkurugenzi nawaagiza hakikisheni mnawasaka usiku na mchana wafugaji wavamizi wanaoingiza na kuharibu mazao kwani haiwezekani watu wachache wavunje sheria ,shirikianeni navyombo vyote vya dola kuhakikisha mnakomesha kabisa tabia hii "

Akitoa ufafanuzi mbele ya mkuu wa mkoa ,mkuu wa wilaya ya mvomero muhamed utaly amsema uongozi wa wilaya kupitia kamati ya ulinzi na usalama tayari umeandaa oparesheni maalum ya kuhakikisha unawasaka na kuwakamata wafugaji wote wavamizi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ili iweze kuchukua mkondo wake,
Utaly amsema  oparesheni hiyo itahusisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama na kudai haiwezekani watu wachache wakoseshe amani na utulivu ulioko ndani ya wilaya na kuahidi watahakikisha watawasaka wavamizi hao usiku na mchana katika oparesheni itakayoanza  hivi karibuni.

Katika hatua nyingine mkurugenzi mkurugenzi wa halmashauri hiyo florent kyombo amewatahazarisha watendaji wa vijiji na kata wanaojihusisha na suala la kupokea rushwa kwa lengo la kuwapokea wafugaji hao kwenye maeneo yao  na atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo hatua kali zitachukuliwa zidi yake ikiwamo kuondolewa kazini.

Kyombo amesema katika hali ya kawaida haiwezekani  mtendaji wa kijiji yupo,mwenyekiti wa kijiji yupo ,na afisa mtendaji wa kata yupo halafu mifugo ingie kwenye vijiji bila taarifa lazima kutakuwa na uzembe ndani yake .

Mkurugenzi huyo amesema watachukua hatua kali kwa watendaji wote wazembe na wasiowajibika au kujihusisha na vitendo vya rusha na miongoni mwa hatua zitakazo chukuliwa ni kwaondoa kazini na si kuwabadirisha vituo vya kazi kama ilvyo zoeleka huko nyuma.
chanzo;.muungwana.

Comments