Mkuu Wa Jeshi La Polisi Nchini, Igp Ernest Mangu Atuma Timu Ya Maofisa Wa Jeshi La Polisi Kwenda Zanzibar Kuchunguza Vitendo Vya Udhalilishaji.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu ametuma timu ya Maofisa wa
Polisi ikiongozwa na Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Alli Mussa kwenda
Zanzibar kushughulikia kero na malalamiko ya wananchi juu ya vitendo vya
udhalilishaji na ukatili kwa watoto/wanawake ambavyo vimekuwa
vikiripotiwa mara kwa mara.
Timu
hiyo imepewa jukumu la kuchunguza vitendo hivyo vya udhalilishaji na
kiini chake na hatimaye kuja na mpango mkakati wa kuzuia vitendo hivyo
ikiwemo kuwakamata wahusika na kuwafikisha mahakamani.
IGP
Mangu amewataka wananchi wa Zanzibar, Taasisi za kiserikali na Taasisi
za kiraia zilizopo Zanzibar kutoa ushirikiano kwa timu hiyo ili
kukomesha vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na maadili ya Watanzania.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
chanzo;mpekuziblog.
Comments