Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma Nhunga wakati wa hafla maalum ya
kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka Mpya wa 2017.
Mh. Mihayo alisema hayo kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyeandaa hafla hiyo Nyumbani kwake Mtaa
wa Kama nje kidogo ya Kaskazini Magharibi ya Mji wa Zanzibar
akiwashukuru baadhi ya Viongozi na Wafanyakazi wa Ofisi hiyo pamoja na
Familia zao walioshiriki katika kuukaribisha mwaka mpya.
Katika kuuaga mwaka 2016 uliobeba matukio mbali mbali yakiwemo mengi
ya udhalilishaji wa Kijinsia ya yale yaliyopoteza maisha ya Wananchi
wengi kutokana na ajali za bara barani, Naibu Waziri Mihayo alisema
suala la kupendana miongoni mwa Jamii ndani ya mwaka mpya wa 2017
linafaa kufanywa kuwa jambo la msingi.
Kupitia hafla hiyo ya chakula cha usiku Mhe. Mihayo Juma Nhunga kwa
Niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwatakia kheir ya mwaka
Mpya Wananchi wote wa Zanzibar na kuwataka wale waliokoseana ndani ya
mwaka uliopita wasameheane.
Alisema Mwaka mpya unahitaji zaidi mambo mapya na ya msingi ili
kulifanya Taifa na wananchi wake waelekee kwenye maendeleo yatakayoleta
faida na kustawisha maisha yao ya kila siku.
Hafla hiyo ya chakula cha usiku uliyowakutanisha baadhi ya Viongozi
na watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Familia
zao iliambatana na muziki laini uliotoa burdani safi kwa washiriki hao
walioshindwa kukaa kwenye viti vyao na kuonekana wakianza kuserebuka.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
1/1/2017.
chanzo; zanzibar24.
Comments