Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la DOTTO MWAIPOPO mkazi wa Kafundo –
Ipinda wilayani Kyela Mbeya ameuawa kwa kuchomwa kisu ubavu wa kulia na
BONIPHACE KISWAGA Mfanyabiashara na Mkazi Chaugingi Mkoani Njombe kwa
madai ya kufanya utapeli.
Taarifa
ya Polisi Mkoa wa Mbeya imesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe
11.01.2017 majira ya saa 4 usiku katika Kitongoji cha Ipinda – Chini,
Kijiji na Kata ya Ipinda, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa
Mbeya.
Inadaiwa
kuwa chanzo cha tukio hilo ni kulipiza kisasi baada ya marehemu
kuwatapeli watuhumiwa pesa ambazo kiasi halisi bado hakijafahamika kwa
madai kuwa yeye ni mganga wa kienyeji na atawasaidia kuwa matajiri.
Aidha
katika tukio hilo mtuhumiwa huyo BONIPHACE KISWAGA alijeruhiwa kwa
kupigwa na wananchi na amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela kwa
matibabu. Watuhumiwa wengine wawili ambao walikuwa pamoja na mtuhumiwa
aliyekamatwa walikimbia na msako mkali unaendelea.
chanzo;mpekuziblog.
Comments