Taarifa kutoka wizara ya ulinzi zinasema Hamza Bin Laden akiwa katika
umri wa miaka ishirini amekuwa kiongozi makini wa kundi la Al Qaeda
ambao ni wapiganaji wa kundi lililoanzishwa na baba yake.
Taarifa
zinasema amekuwa makini katika suala hilo kwa kufuata nyayo za baba yake
kwa kujiunga na jihadi na kusambaza ujumbe wa sauti kwa niaba ya kundi
la Al Qaeda na kuchochea mashambulizi dhidi ya nchi za Magharibi.
Kwa sasa Atazuiliwa kufanya biashara na wananchi wa Marekani na mali zake zitataifishwa.
Kiongozi mkuu wa usalama wa kundi la Al Qaeda Ibrahim al-Banna ametajwa katika orodha hiyo pia.
Marekani itatoa ofa ya dola Million tano kwa atakayesadia kukamatwa kwa al-Banna.
chanzo;bbc.
Comments