Hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi yake kubwa aliyoiweka wakati wa kampeni za uchaguzi.
Akizungumza
na wafanyakazi wanaohusika na usalama wa taifa, Donald Trump amesema
ukuta huo utazuia wahamiaji haramu na wafanyabiashara wa dawa za
kulevya, kwa kuongeza kuwa siku zao zimekwisha wao kuishi na kufanya
uharibifu.
Amesisitiza kauli yake ya kutaka Mexico kulipia ukuta huo, licha ya Mexico kukataa kufanya hivyo.
Wakati Marekani ikiweka msimamo wake huo, serikali na raia wa Mexico nao wameingilia kati kutetea nchi yao.
Rais
wa Mexico Enrique Pena Nieto naye anashinikizwa kufuta mkutano wake na
Rais Trump unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo mjini Washngton, ikiwa kama
ni kujibu uamuzi huo wa Marekani kujenga ukuta.
Meya wa mji wa
Mexico City Miguel Espinosa amesema kujengwa kwa ukuta huo, Marekani
itajitenga yenyewe sio tu na Mexico bali na Amerika ya kusini yote.
Wakati
huohuo, Rais wa Marekani amesema kuwa ana amini kwamba njia ya mateso
inayotumika kuwahoji washukiwa wa ugaidi inafanya kazi vilivyo.
Akihojiwa
na kituo cha Televisheni cha ABC, amesema Marekani inapaswa kupambana
kwa nguvu zote katika kujibu mateso yaliyofanywa na kundi la Islamic
State kwenye eneo la mashariki ya kati.
Mtangulizi wake Rais
Barack Obama alipiga marufuku njia hiyo ya kutumia maji kuwahoji
washukiwa kutokana na kuleta mabishano, mbinu hiyo ilikuwa ikitumika
wakati wa utawala wa George Bush.
chanzo;bbc.
Comments