Maradhi yasiyopewa kipaombele yataka kutokomezwa Zanzibar.

Wizara ya Afya Zanzibar kupitia kitengo cha maradhi ya yasio pewa kipaumbele (kichocho,matende, na Vikope)kimo katika harakati za kuyatokomeza kabisa maradhi hayo katika maeneo ya Zanzibar.
Hayo yamesemwa leo huko Mkoa wa Kusini Unguja katika Hoteli ya visital inn Jambian na Dr.wa maradhi hayo Khalifan Abdalla Mohamed wakati wa semina ya mapitio wa mradi uliomaliza wa kuyatokomeza maradhi hayo.
Amesema maradhi ya kichocho na matende yaliathiri sana wananchi wa visiwa vya zanzbar katika miaka ya thamanini na kupelekea wengine kupata maradhi ya matende hadi hii leo jambo ambalo kwasasa maradhi hayo yanaonekana kutoweka kutokana na jitihada za Serikali na washirika wake wa maendeleo kulivalia njuga tatizo hilo.
Amsema kwa sasa hali hiyo inaridhisha kwakiasikikubwa na sehemuzilizo bakia nichache kuliitokomeza tatizohilo
“Tuna tarajia kuyamaliza maradhi ya kichocgo na matende kwani imekuwa nadra kupokea wagonjwa wamaradhi haya ispokuwa niwale wale wagonjwa wazamani tu walioathirika na matende,kichocho,na  zipo baadhi ya maeneo ambayo hayajamalizika maradhi hayo kama vile kamgamba,kinyasini,moga,kizimkazi na kwapemba micheweni kwa”alisema DR Khalifan.
Nae mwenyekiti wa mradi wa kutokomeza maradhi hayo kutoka Nchini giniva katika shirika Global Schistosomiasis Alliance Dr Lorenzo Savioli amesema mapitio ya semina hiyo ni kuangalia vipi kuisaidia Zanzibar  kwa kuwapatia madawa na kufikia lengo la kuyatokomeza maradhi hayo.
Amsema  wananchi wazitumie dawa hizo kwa rika zote na hazina matatizo yoyote bali zinapoza zaidi maradhi mengine kama vile mapele mabaka na mipasuko mwilini.
Alisema wazitumie dawa hizo bure na nifrusa kwao ,kwani nchini kwao dawa hizo ni ghali mno kwa mwananchi wa Tanzania.
Nae mkurugenzi wa Maendeleo ya maji Zanzibar Muhamed Iliasa Mohamed alisema katika kuondoa tatizo la kichocho Zanzibar ni kuhakikisha kupeleka maji safi na salama katika maeneo yote ya zanzbar ili wananchi waweze kutumia maji safi na kuacha kutumia maji ya mito na mashimo.
Aidha alisema wanalazimika maji kuyatia dawa yakuulia vimelea vya maradhi hayo ili visiwe na nafasi ya kuathiri wananchi wanapo yatumia.
chanzo;zanzibar24.

Comments