Fainali
za 11 za michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup zinatarajiwa kupigwa leo
kwenye dimba la Amaan Visiwani Zanzibar kwa kuzikutanisha timu za Simba
na Azam zote za Dar es Salaam.
Mchezo
huo unaotarajiwa kuanza Saa 2:15 usiku wa leo, utakuwa ni wa pili
kuzikutanisha timu hizo katika fainali ya michuano hiyo.
Awali
zilikutana katika fainali ya mwaka 2012 na Azam FC ikaibuka na ushindi
wa mabao 2-1 na kutwaa taji lake la kwanza kati ya mawili ya Kombe la
Mapinduzi, linguine likija mwaka 2013 baada ya kuifunga Tusker katika
fainali.
Simba
ndiyo mabingwa mara nyingi wa taji hilo, mara tatu baada ya kulitwaa
katika miaka ya 2008 ikiifunga Mtibwa Sugar katika fainali, 2011
ikiwafunga mahasimu, Yanga na 2015 wakiwafunga Mtibwa Sugar.
Kocha
wa Simba Joseph Omog, amepania kulitwaa taji hilo, kwa lengo la kuondoa
ukame wa makombe ambayo umeikumba klabu hiyo kwa misimu minne iliyopita
pasipo kubeba ubingwa wowote
Azam
mara zote ilizoingia fainali ilitwaa taji hilo, wakati Simba mwaka 2012
na 2014 ilicheza mechi ya mwisho na kufungwa na kukosa Kombe hilo.
Kuelekea
mchezo wa leo, kila timu iko vizuri baada ya rekodi nzuri katika mechi
zilizopita, Simba wakiwatoa wapinzani wa jadi, Yanga kwa penalti 4-2
baada ya sare ya 0-0 kwenye Nusu Fainali na Azam wakiitoa Taifa
Jang’ombe kwa bao 1-0.
Timu
zote ziliongoza makundi yao, Simba A lilikuwa na timu tano kwa pointi
zake 10 na Azam B lililokuwa na timu nne kwa pointi zake saba.
chanzo;mpekuziblog.
Comments