Kauli hiyo ameitoa leo huko Michakaeni wilaya ya chakechake mkoa wa kusini Pemba wakati alipokua akifungua jengo jipya la Ofisi ya Baraza la Mji wa Chake Chake.
Waziri Aboud amefahamisha kua kuna baadhi ya wananchi wanaoneakana bado hawajui umuhimu wa kua na umoja katika nchi na wapo ambao pia hawaithamini seriakili iliyopo madarakani kwa mitazamo ya kisasa hivyo amewataka wananchi wote kwa pamoja kuwa kitu kimoja ili kupigana na maendeleo na kuleta mafanikio kwa watu wote kwa ujumla.
Aidha Mh Aboud amesefahamisha kua kuna baadhi ya maeneo kumekua na vitendo vya hujuma vinaendelea kujitokeza ikiwemo watu kuchomeana moto vitu vyao pamoja na kukatiana mazao na vipando kwa mitazamo mibaya ya kisiasa.
Amesema kama ni uchaguzi umeshamalizika na raisi aliyechaguliwa kihalali ni Mh Dk Shein hivyo vitendo vya hujuma haviwezi kumuondoka madarakani.
Mapema akimkaribisha Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mheshimiwa Mwanajuma Majidi Abdalla katika ufunguzi huo amewataka wafanyabiashara kufanya biashara zao vizuri na kufuata taratibu zilizo wekwa kwa lengo la kulikuza Baraza la Mji wa Chake Chake
lengo la kujengwa jengo hilo ni kuwajali na kuwathamini wafanyakazi wa baraza hilo ili kua katika mazingira mazuri hatiame kupatiakane ufanisi wa kutosha katika utendaji wa kazi.
Comments