Mgomo huo umelemaza huduma katika hospitali na zahanati za umma.
Rais
Uhuru Kenyatta alikutana na wawakilishi wa chama cha taifa cha
madaktari hao Jumanne na kupendekeza nyongeza ya mshahara na marupurupu
ya madaktarii kwa angalau $560 (£450).
Hilo lingesababisha madaktari wanaoanza kazi kulipwa takriban $2,000 kila mwezi.
Viongozi
wa chama hicho, ambao walikuwa wameahidi kutangaza msimamo leo,
walisema pendekezo la serikali linawafaa madaktari lakini kuna baadhi ya
mambo ya kuwafaa wananchi ambayo yameachwa nje.
Madaktari wanaitaka serikali kutekeleza makubaliano ya mishahara na marupurupu yaliyotiwa saini mwaka 2013.
Kwenye makubaliano hayo, serikali iliahidi kuongeza idadi ya madaktari,
kuongeza pesa za utafiti wa kimatibabu, dawa na vifaa na mitambo katika
hospitali za umma.
CHANZO;BBC.
Comments