Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya rais na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi,Issa Haji Ussi wakati wa uzinduzi wa awali
kutambuisha huduma ya 4G LTE Zanzibar huko Kijangwani mjni Unguja.
Amesema Serikali imekuwa ikishajihisha wawekezaji kuwekeza hivyo kuimarishwa kwa huduma ya 4.G yaTTCL kunatokana na juhudi za Serikali ya Tanzania kuunga mkono huduma za mawasiliano kwa wananchi wake.
Nae kaimu afisa mtendaji mkuu TTCL Waziri Kindamba amesema kutokana
na kampuni hiyo kuwa mama, watahakikisha ndani ya kipindi cha mwaka
mmoja mawasiliano yanaimarika katika sehemu zote.
Aidha Kindamba amewaomba wananchi kutambua kuwa huduma za TTCL
zinapatikana kupitia simu za mezani na mkononi hivyo ni vyema wananchi
kuunga mkono juhudi za kuimarisha mawasiliano.
chanzo:Zanzibar24
Comments