
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Zanzibar Bw. Joseph Meza (wa
kwanza kulia) akiongoza kikao kazi cha Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katikati ni Mwenyekiti Mwenza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof.
Faustin Kamuzora. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Muungano kutoka
Ofisi ya Makamu wa Rais Dar es Salaam Bw. Baraka Rajab. Kikao kazi hicho
kimefanyika leo tarehe 05/01/2017 katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar na kwa pamoja wamejadili changamoto za Muungano.
Baadhi
ya Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
wakifuatilia kikao kazi kilichojadili changamoto za Muungano. Kikao
hicho kimefanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar.
Bw.
Shomari Omar Shomari Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na
Usafirishaji, Bi. Fatma Gharib Bilal Katibu Mkuu Kazi, Uwezeshaji,
Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto na Bi. Khadija Bakari Juma Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali kwa pamoja wakifuatilia kikao kazi
kilichojadili changamoto za Muungano na namna bora ya kuzipatia
ufumbuzi.
Mwenyekiti
na Mwenyekiti Mwenza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais –
Zanzibar Bw. Joseph Meza (wa pili kulia) na Prof. Faustin Kamuzora (wa
tatu kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu
kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi.
Pichani
ni Mwenyekiti na Mwenyekiti Mwenza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili
wa Rais – Zanzibar Bw. Joseph Meza (wa pili kulia) na Prof. Faustin
Kamuzora (wa tatu kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na
Sekretarieti iliyoratibu kikao hicho ikiwa na wajumbe kutoka Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
chanzo; .zanzinews.
Comments