Ziara ya Wajumbe wa Kamati ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya
Wanawake ya Baraza la Wawakilishi iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Dkt.
Mwinyihaji Makame katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)
iliyofanyika tarehe 24 Januari, 2017.
Lengo la ziara hiyo ni kuangalia
utekelezaji wa majukumu ya Serikali yanayofanywa na Wizara mbalimbali.
Wakiwa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, ambacho kiko chini ya Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Amali walifanya mazungumzo na Baraza la Chuo
chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Said Bakari Jecha.
Mheshimiwa Mmanga
Mjengo Mjawiri, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali pia
alishiriki katika ziara hiyo.
chanzo;zanzibar24.
Comments