Kaka alawiti ndugu wake wawili waliozaliwa tumbo moja.

Mtu mmoja aliefahamika kwa jina la  Mohd Ali Juma mwenye umri wa miaka 27  mkaazi wa tomondo amefanya tukio la kikatili la kuwalawiti ndugu zake wawili waliozaliwa tumbo moja.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea huko tomondo Wilaya ya Magharibi B Unguja ambapo mtuhumiwa huyo aliwabaka ndugu zake hao wawili mmoja ana umri wa miaka 12 na mwengine ana umri wa miaka 13 wote ni watoto wa kiume na majina yao yamehifadhiwa.

Mama mzazi wa watoto hao alisema kuwa watoto hao walikua wanalala na kaka huyo nyumba  moja ndipo alipoata wasaa wa kuwafanmyia kitendo hicho cha kikatili hivyo mama huyo  aliitaka serikali kutolifumbia macho suala hilo badala yake wamchukulie hatua kali za lkisheria.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Mjini Magharibi kamishna msaidizi muandamizi wa polisi Hassana Nassir ali amesema mazingira ya kaka kuwaingilia ndugu zake ni mazingira hatari ambayo  hayakuzoeleka katika Nchi yetu hivyo aliitaka jamii kujirekebisha na kutoa ushirikiano  yanapotokea matukio kama hayo.

chanzo; zanzibar24.

Comments