Mia Ahmad Fatty amewaambia
Waandishi wa habari katika mji mkuu wa Senegal Dakar kwamba wataalamu wa
masuala ya fedha wanatathmini kujua ni kiasi gani kwa sasa kimepotea.
Amesema Gambia kwa sasa ina tatizo kubwa kifedha kwa hazina yake kutokuwa na kitu.
Kwa sasa Rais Barrow amekuwa akifanya kazi na timu ya wataalamu wa
masuala ya fedha na wengine kutoka Benki kuu ya nchi hiyo kupata kiasi
halisi kilichopo.
Habari zinasema magari ya kifahari na mali
nyingine zilionekana zikipakiwa katika ndege ya mizigo ya Chad kwa niaba
ya Rais Jammeh siku alipoondoka nchini humo.
Maelfu ya watu
walikusanyika katika Ikulu ya nchi hiyo jana jioni wakiyaangalia majeshi
ya Senegal yakiingia kwa ajili ya kuweka usalama kabla ya kurejea
nchini kwa Adama Barrow.
Rais Barrow yupo nchini Senegal na bado haijulikani ni lini hasa atarudi Gambia na kuingia ofisini.
chanzo:bbc.
Comments