Hafla hiyo ilifanyika jana katika kampasi ya SUZA, Tunguu wilaya ya Kati Unguja.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Balozi mdogo wa china Zanzibar
Xie Xiawou alisema, msaada huo utasaidia ununuzi wa vifaa kama
televisheni na ving’amuzi ili kuwajengea uwezo walimu wa chuo hicho
katika kutengeneza vipindi bora vya elimu kwa wanafunzi.
Aidha alisema uhusiano uliopo kati ya Zanzibar na China unasaidia
kuimarisha maendeleo kwa zanzibar kutokana na miradi mingi inayotolewa
kwa ajili ya Zanzibar. Nae makamo mkuu wa chuo hicho Prof. Idris Ahmada
Rai Alisema SUZA itachagua baadhi ya skuli za sekondari kuzifungia
televisheni na ving’amuzi ili kuwawezesha wanafunzi wa Sayansi, Hisabati
na Kingereza kujifunza moja kwa moja kupitia televisheni hiyo.
Pia aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo na kusema sehemu
iliyobakia ya fedha hizo zita tumika kama motisha kwa walimu ilikuongeza
kasi ya maendeleo ya elimu katika chuo hicho na Zanzibar kwa ujumla.
Waziri wa elimu na mafunzo ya amali, Riziki Pembe Juma aliishukuru
serikali ya china kwa jinsi inavyo shiriki kikamilifu kuimarisha
maendeleo ya elimu Zanzibar na kwa kuijengea uwezo televisheni hiyo ya
suza ili kujenga uwezo kwa wanafunzi wa Zanzibar.
Nae mkurugenzi mtendandaji wa Huawei Tanzania Kanef Luo alisema
teknolojia ya mawasiliano ni muhimu katika taasisi za elimu hivyo
kampuni yake itaendelea kushirikiana na Zanzibar kuhakikisha inapiga
hatua nzur katika matumiz ya teknolojia hiyo katika kizazi kijacho.
Kituo cha televisheni cha Suza kinakua ni kituo cha kwanza Tanzania
kujikita moja kwa moja katika kuandaa vipindi vya elimu ambapo wanafunzi
watapata fursa ya kufuatilia mada ambazo zimo kwenye mitaala yao.
Chanzo: Zanzibar Leo na zanzibar24.
Comments