Hitilafu Grid ya Taifa.

Tanesco, Makao makuuMaeneo yote yaliyounganishwa kwenye mfumo wa taifa wa kusambaza umeme Tanzania asubuhi yameathiriwa na kukatika kwa ghafla kwa umeme.
Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania limesema tatizo hilo limesababishwa na hitilafu katika mtambo wa kupooza na kusambaza umeme eneo la Ubungo, Dar es Salaam.
Umeme ulikatika mwendo wa saa kumi na mbili unusu asubuhi.
Kaimu meneja uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji amenukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema wataalam wanaendelea kushughulikia tatizo hilo.
“Tatizo hili limetokea leo saa 12:32 asubuhi katika mtambo wa kilovolti 220 ambao ni wa kupoozea na kusambaza umeme uliopo Ubungo lakini kwa kuwa wataalam wameshagundua,” Muhaji ameambia Mwananchi.
Kufuatia hitilafu hiyo Shirika la umeme limetoa taarifa rasmi inayohusu ya shirika
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
TAARIFA YA KUTOKEA KWA HITILAFU KATIKA GRID YA TAIFA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake na Umma kwa ujumla kuwa kumetokea hitilafu katika Kituo kikubwa cha kupoza na kusambaza Umeme cha Ubungo, hitilafu hiyo imesababisha Grid ya Taifa kutoka na kusababisha Mikoa yote iliyounganishwa katika Grid ya Taifa kukosa Umeme.
Mafundi wanaendelea na jitihada ya kurejesha Umeme katika hali yake ya kawaida.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza.
Imetolewa na; Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu.
chanzo;zanzibar24.

Comments