SWALI: Zanzibar imetimiza miaka 53 ya Mapinduzi una lipi la kuwaeleza Wazanzibar?
JIBU:
Unapoongelea Mapinduzi ya Zanzibar, wote tukumbuke ndio chanzo cha
Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar, bila Mapinduzi Muungano
usingekuwepo, haya yote ni katika kuzingatia umoja. Umoja ni jambo la
msingi sana kwa Wanzanzibar kwa kuwa Serkali ya Kikoloni ilitubagua na
kupanda mbegu ya kubaguana hata kwa sisi Wafrika wenyewe.
Ni vema kuyaenzi Mapinduzi haya kwa kuwa ndio chanzo cha Muungano
wetu, Amani yetu, Umoja wetu, Utulivu wetu na Mshikamano wetu. Hivyo
tunakila sababu ya kushukuru uwepo wa Mapinduzi ya mwaka 1964 yameweza
kutuunganisha tukawa na Umoja.
Awamu ya kwanza ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar Marehemu Shekhe Abeid
Amani Karume alifanya mambo mengi makubwa mfano ujenzi wa nyumba bora
za makazi za wananchi, kutoa elimu bure, huduma za afya, maji na
kufuta kabisa ubaguzi wa kila aina ambao ulikuwa umeota mizizi hapa
Zanzibar kabla ya Mapinduzi.
Aidha, Awamu ya pili Serikali ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais wa
Zanzibar Mheshimiwa Marehemu Abood Jumbe, iliandika Katiba ya Zanzibar,
kuundwa kwa Baraza la Wawakilishi, kutengeneza muundo wa Baraza la
Wawakilishi na kuanza kazi kwa kuwa na wakikilishi Zanzibar na Katika
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Awamu ya tatu mpaka ya Saba ni
muendelezo wa:
Tatu, Uchumi wa Zanzibar umekua, kama kuzalisha mazao zaidi hapa
visiwani, mfano asilimia 80 ya matunda yalikuwa yanatoka Tanzania Bara
lakini sasa katika Awamu ya saba ya Mheshimiwa Dkt Ali Mohammed Shein,
uzalishaji wa matunda umeongezeka asilimia 80 inatoka Zanzibar na 20 tu
ndio yanatoka Tanzania Bara.
Ujenzi wa barabara kila mkoa, miundombinu mbalimbali imeongezeka kama
hospitali, bandari imeimarishwa ambapo kwa sasa kuna meli nyingi zaidi
za mizigo na Uvuvi ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Nne, suala la kubadilishana uongozi kutoka awamu ya kwanza mpaka ya
saba, tofauti na uongozi wa kisultani ambao ulikuwa ni wakurithi kutoka
kizazi kimoja hadi kingine katika familia moja tu.
SWALI: Mheshimiwa Hamad Rashid wewe ni kati ya watu wachache
waliobobea katika siasa na umeitumikia Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, na Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Unadhani
muelekeo uliopo mpaka sasa unaleta hali halisi ya matarajio ya Mapinduzi
yaliyofanyika mwaka 1964?.
JIBU:
Muelekeo upo na madhumuni makubwa ya mapinduzi ni kutaka kujitawala
wenyewe, unapojitawala utaepuka kudharauliwa, kunyanyaswa na kuondoa
ubaguzi uliokuwa umekithiri katika utawala wa Wakoloni enzi hizo.
Pili makazi na maisha ya Wanzanzibar waliowenngi yalikuwa duni na
umaskini ulikuwepo wa hali ya juu kwa jamii za kiafrika na; Tatu Uchumi
wa Zanzibar ulikuwa mikononi mwa wakoloni hakuna Mzanzibar aliyeruhusiwa
kumiliki sehemu ya uchumi wa nchi. Kutokana na kadhia hiyo utamaduni
wetu ulidharauliwa utu wetu ulipuuzwa na ushiriki wetu wa uchumi ulikuwa
haupo.
Hivyo madhumuni makubwa ya mapinduzi ni kuleta umoja, usawa, utulivu
na mshikamano miongioni mwa wanzanzibar hilo limefanikiwa kwa asilimia
kubwa ukilinganisha na hali ya mwaka 1964.
SWALI: NIni maoni yako kuhusu Serikali ya Mapinduzi ya Zanznibar kuelekea kwenye uchumi wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa?.
JIBU:
Tukubali kuwa uchumi ndio msingi wa maendeleo wa Taifa lolote. Sera
zinazoandaliwa ni lazima zilenge katika kuleta maendeleo ya nchi
kiuchumi. Rais anaposema anataka Taifa liondokane na umasikinini ni
kweli tutaondokana nao, kama tutakuwa na viwanda vichache vyenye manufaa
kwa nchi kwa kuwa eneo la kisiwa ni dogo. Hivyo, tutaongeza ajira
Wakulima watapata soko la uhakika la mazao yao na bidhaa
zitakazozalishwa zitauzwa ndani na nje ya nchi kwa kuwa zimeongezewa
dhamani.
Ni vema Wazanzibar tukadhamini vitu vinavyozalishwa nchini mwetu na kupenda kushiriki katika kufanya kazi.
SWALI: Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inalipi la kujivunia katika miaka 53 ya Mapinduzi Tukufu ya Zanzibar?.
JIBU:
Yapo mengi ya kujivunia, leo hii hakuna wakutupuuza, kutudharau na
kutunyanyasa, tunatembea kifua mbele kwa marefu na mapana katika kila
jambo liwe lakijamii, kiuchumi, elimu, miundombinu, afya, michezo au
utamaduni kila Mzanzibar ana haki ya kushiriki katika maendleo ya
Zanzibar. Hapa la msingi kila Mzanzibar ajiulize atafanya lipi kwa
Zanzibar ili kuleta maendeleo, kila raia anatambua maendeleo yetu
yataletwa na sisi wenyewe. Maana ukitaka au kudai haki lazima ujue
wajibu wako kwa nchi katika kuleta maendeleo.
Mambo ya msingi ya kujivunia yanabaki kuwa ni Umoja wetu, Mshikamano
wetu Amani yetu, Utulivu wetu na hali ya kuvumiliana katika siasa hasa
uvumilivu wa kufanya siasa za vyana vingi.
SWALI: Suala la Nidhamu kwa Watumishi wa Umma, Taasisi, Mashirika na
Idara za Serikali linatiliwa mkazo sana na Rais wa Zazibar Mheshimiwa
Dkt. Ali Mohammed Shein hili unalizungumziaje?.
JIBU:
Ni kweli Mheshimiwa Rais Dkt. Ali Mohammed Shein, anasisistiza
nidhamu na kufanya kazi kwa bidii na kujituma. Amesema kabisa hataki
tufanye kazi kwa mazoea, anasisistiza kabisa kwenda kwa wananchi na
kufanya kazi nao ili kujua wanachofanya, changamoto zao ili viongozi
waweze kuzitatua pamoja na wananchi. Anatuhimiza tutoke tuende kwa
wananchi na kuona ni jinsi gani tunaweza kufanya nao kazi kwa pamoja ili
kuleta maendeleo bila kubagua rangi, kabila, dini, Jinsia na uwezo.
ADC tunasema asilimia 70 kazi na asilimia 30 tutakaa maofisini. Kwa
sasa watumishi wote waone umuhimu wa kufanya kazi badala ya kupiga
maneno maneno tu, tabia hii haitatusaidia Wazanzibar.
SWALI: Nini nafasi ya Vyama vya Upinzani katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar?.
JIBU:
Vyama vya Upinzabni vina nafasi kubwa katika Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar na nje ya serikali katika masuala muhimi kwa wananchi ya
kuleta maendeleo. Nitakupa mfano binafsi na chama chetu cha “Alliance for Democratic Change” – ADC tulishirikiana na wananchi kutafuta wafadhili kama chama cha siasa na kujenga uwanja wa mpira Pemba sikuwa Waziri wala Diwani.
Pia ni fadhaa kumsingizia Mheshimiwa Rais eti hatoi nafasi kwa vyama
vingine vya siasa. Mimi mwenyewe nipo ndani ya serikali tunakaa kwenye
vikao mpaka saa 6 usiku kila mhusika natoa mawazo yake katika kuwaletea
maendeleo Wazanzibar. Kama hoja unayotoa ni ya msingi lazima
itakubalika, inapofikia suala la maendeleo Mheshimiwa Rais Shein
haangalii chama anaangalia masilahi ya Zanzibar kwanza.
Kila Mzanzibar ana wajibu wa kujiuliza ameifanyia nini Zanzibar ili
kuleta maendeleo na sio kusifiwa kwa malumbano ambayo hayana masilahi
kwa maendeleo.
SWALI: Ni kweli Serikali ya SMZ Ikiongozwa na Chama cha Mapinduzi –
CCM inakandamiza demokrasia na kubagua Vyama Vingine vya siasa?.
SWALI:
Ni kweli Serikali ya SMZ Ikiongozwa na Chama Tawala cha CCM inakandamiza demokrasia na kubagua Vyama Vingine?.
JIBU:
Hili la kubaguliwa na kukandamizwa demokrasia halina ukweli hata
kidogo, Katika Awamu ya kwanza ya uongozi niliwahi kupendekeza jambo
ambalo idadi kuwa ya washiriki walilikataa, lakini kutokana na uzito wa
hoja, Serikali ililipima na kulichukua hii ndio demokrasia, kama suala
lina masilahi kwa nchi ni vema likafanyika kwa masilahi ya nchi.
Mimi ni mwanachama wa “Alliance for Democratic Change” katika
utendaji wa kazi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Shein sijawahi kubaguliwa au kutengwa kwa
sababu natoka chama kingine cha sIasa.
Mhe. Rais anatushirikisha katika kila jambo na katika vikao tunaongea
na kutoa mawazo na mapendekezo yetu ambayo yanachukuliwa na kufanyiwa
kazi kama ambavyo yangeweza kutolewa na muwakilishi wa chama chake cha
CCM.
SWALI: Una wito gani kwa wanzanzibar na Watanzania kwa ujumla?.
JIBU:
Mosi, Umoja wetu, Usawa kwa kila Raia na Mshikamano wetu ni masuala ya msingi sana katika nchi yetu.
Pili, tunataka nchi hii ibaki salama, mnapokuwa na amani katika nchi
yenye rasilimali za kutosha mtaweza kujipanga vema na kuzitumia
rasilimali hizo kwa faida ya wote, hivyo ni lazima tuhakikishe kuna
Amani na pale wachache wanapohatarisha amani hiyo kwa pamoja
tushirikiane kusuluhisha ili kurejesha hali ya utulivu na amani.
Serikali ipo imara katika kuleta Maendeleo lakini wewe Mzanzibar ni
lazima utimize wajibu wako. Mfanya biashara alipe kodi na afanye
biashara ya halali. Mkulima afanye kazi kwa bidii na Serikali ihakikishe
inampatia pembejeo kwa wakati na zenye ubora.
Tatu, sisi wanasiasa njia za kurekebisha makosa zipo tukubali kukaa
chini na kuzungumza, lawama hazina nafasi, Chama cha siasa ni lazima
kuwa na mipango ya maendeleo na mipango hiyo ifanyike hata kama hauko
katika uongozi.
Nne, tunao viongozi wetu wa dini kama Mashekhe, Mapadri Wachungaji
tuwe karibu nao tuongee nao waweze kutuelekeza pale tunapokosea na
kwenda katika mwenendo sahihi. Mwisho nawapongeza kwa dhati kabisa
Wazanzibar kutimiza miaka 53 ya Mapinduzi.
chanzo; zanzibar24.
Comments