Guterres: Mitazamo inayowabagua Waislamu inahuzunisha sana.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema jumuiya hiyo ya kimataifa ina wasiwasi mkubwa kuhusu ubaguzi unaowalenga wahajiri na jamii za waliowachache.
António Guterres amesema, kwa sasa mitazamo ya taasubi inaenea kwa kasi na kufungua njia ya chuki na uadui, hivyo jamii ya kimataifa inalazimika kuwa makini na macho.
Guterres amesema Umoja wa Mataifa unapaswa kuimarisha taasisi zake katika masuala ya haki za binadamu na vilevile kutekeleza uadilifu dhidi ya wale wanaofanya jinai kubwa dhidi ya binadamu.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema mitazamo ya kibaguzi ambayo hii leo inawalenga Waislamu inahuzunisha sana. 
Matamshi hayo ya António Guterres yametolewa wakati Rais mpya wa Marekani, Donald Trump amezidisha siasa zake za kibaguzi na kiadui dhidi ya wahajiri na Waislamu.
Ijumaa ya jana Trump alitia saini amri ya kuwazuia Waislamu kuingia nchini humo. Wakati wa kampeni zake za uchaguzi, Trump alitoa wito wa kuzuiwa kikamilifu Waisalmu kuingia Marekani.  
chanzo:parstoday.

Comments