Fedha za awamu ya kwanza ya ujenzi wa jengo hilo zilikuwa ni za mkopo
kutoka katika Benki ya HSBC, na katika awamu ya pili serikali
inatarajia kutumia Euro 121,634,888 (sawa na Sh bilioni 290.2)
kukamilisha ujenzi huo.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Profesa Makame Mbarawa wakati alipotembelea uwanjani hapo ili kufanya
ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi huo unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa
mwaka huu.
“Awamu ya kwanza ilikuwa ni mkopo lakini awamu ya pili Serikali
tumesema hatutachukua mkopo, tutalipa kwa pesa zetu za Kitanzania,”
alisema Profesa Mbarawa.
Alisema utaratibu wa kujenga uwanja huo kwa pesa za ndani si wa
kwanza kwani kuna miradi mingi na hasa katika sekta ya barabara ambayo
inatekelezwa kwa utaratibu huo.
Awali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA),
Salim Msangi alisema mradi huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo fedha za kulipia Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) .
chanzo;habarileo.
Comments