Wakati
Wazanzibari leo wakiadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar, Rais wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein (pichani),
amebainisha kuwa mapinduzi hayo ndio alama, sifa, ukombozi na uhuru wa
raia hao wa visiwa vya Zanzibar.
Dk Shein amesema hana ugomvi na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya CUF katika uchaguzi mkuu wa mwaka juzi na kubainisha kuwa wanatofautiana kisiasa, ni jambo la kawaida na mazungumzo ya muafaka yalishafanyika.
Pamoja na hayo, Rais huyo amebainisha kuwa anaamini amechaguliwa kihalali na Wanzanzibari, ambapo kufutwa na kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar mwaka 2015, hakukuwa na shinikizo lolote kutoka serikalini bali ni maamuzi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) baada ya kubaini mchezo mchafu kwenye uchaguzi huo.
Dk Shein amesema hana ugomvi na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya CUF katika uchaguzi mkuu wa mwaka juzi na kubainisha kuwa wanatofautiana kisiasa, ni jambo la kawaida na mazungumzo ya muafaka yalishafanyika.
Pamoja na hayo, Rais huyo amebainisha kuwa anaamini amechaguliwa kihalali na Wanzanzibari, ambapo kufutwa na kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar mwaka 2015, hakukuwa na shinikizo lolote kutoka serikalini bali ni maamuzi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) baada ya kubaini mchezo mchafu kwenye uchaguzi huo.
Akizungumza
katika kipindi cha Funguka kilichorushwa na Azam TV jana usiku, Dk
Shein alisema kilichohitajika ni mazungumzo ya pande mbili ambayo
yalifanyika baina yao na mwelekeo ulikuwa mzuri lakini Maalim Seif
hakutaka kurudia uchaguzi.
Mvutano
huo ulijitokeza wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 baada ya
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta
matokeo hayo na kusababisha mvutano wa kisiasa kabla ya kutangaza
kurudiwa Machi 20, 2016, ambao CUF iligoma kushiriki.
Katika mahojiano hayo, Dk Shein alisema, “Mimi
nilikuwa mwenyekiti wa mazungumzo yale na Maalim upande wa pili huku
wajumbe wakiwa marais wastaafu, Ally Hassan Mwinyi, Aman Karume na
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd.
“ZEC
ni tume huru na inayojisimamia kwa mujibu wa sheria na Katiba ya
Zanzibar, taasisi yoyote haiwezi kuiingilia hata kama ni Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC), ndiyo maana wao (NEC) hawakuona dosari katika
uchaguzi lakini ZEC waliziona na kutoa sababu tisa za kufuta uchaguzi,” alisema Dk Shein.
Alisema
uchaguzi wa Zanzibar umekuwa na matatizo tangu mwaka 1957 na wa awamu
hii, Tume ilikuwa na hoja za msingi kuurudia huku akisema mwenyekiti wa
Tume anateuliwa na Rais kwa mujibu wa Katiba na si kwa ajili ya
kumpendelea.
Changamoto za Muungano
Dk
Shein alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizofanikiwa katika
kudumisha Muungano na changamoto zake pekee anazozitambua ni tume ya
pamoja ya fedha na suala la mafuta ambalo limepatiwa ufumbuzi.
“Kabla
ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa kelele za Muungano na muundo wa
Serikali hazikuwahi kusikika lakini baada ya baadhi ya wanaCCM
kuenguliwa na kuhamia upande wa pili, ndiyo walioanza kuwalisha watu
sumu. Lakini anayeupinga Muungano haijui asili yake,” alisema Dk Shein.
Mchakato wa Katiba
Alipoulizwa
kuhusu Katiba mpya baada ya Rais John Magufuli kusema hicho si
kipaumbele chake, Dk Shein alisema hayo ni masuala ya kushauriana baina
ya viongozi hao wawili.
“Mchakato
wa Katiba tuliuanza mimi na Jakaya Kikwete (Rais mstaafu) na ile Katiba
ni ya Muungano, hivyo jambo lolote ni lazima viongozi wa Serikali mbili
washauriane. Mambo haya si ya kulazimisha...,” alisema.
Uongozi wa Magufuli
Rais huyo alisema anamfahamu Rais Magufuli tangu akiwa waziri na anajua uwezo wake, “Majipu
anayoyatumbua Rais habahatishi kwani anafanya vile kwa mujibu wa katiba
na sheria za nchi, na si kwamba mimi situmbui, natumbua sana, sema mimi
staili yangu siyo ya kusema kila kitu na waandishi wa huku (Zanzibar)
si wafuatiliaji sana kama wa Bara,” alisema Dk Shein.
Aliongeza
kuwa watu hawawezi kujua utumbuaji wake kama waandishi wa habari si
wafuatiliaji, vilevile hawezi kuyajua majipu zaidi kama waandishi wa
habari hawajayaibua, “Waandishi wa habari wa Zanzibar ni tofauti sana na
wa Bara.”
Akizungumzia kauli ya Rais Magufuli kuwa awe mkali, Dk Shein alisema, “Kwa
kuzungumza mimi ni mpole lakini mtu akikosea, mimi ni mkali kwelikweli,
sema mimi siyo mtu wa kukasirika ovyo, busara zinaniongoza sana,
japokuwa ukikosea sikuachi hata kidogo,” alisema Dk Shein.
Alisema katika kipindi chote ambacho amekaa madarakani, anajivunia kuifanyia Zanzibar mambo mengi na bado anaendelea.
“Katika
utawala wangu nimeanzisha mpango wa elimu bure kuanzia shule ya msingi
mpaka sekondari, sasa wazazi wanachangia ada ya mitihani tu ya kidato
cha nne na cha sita na yenyewe muda si mrefu nitaiondoa,” alisema Dk Shein.
Kuhusu
afya, alisema licha ya Wazanzibari wengi kutibiwa nje ya visiwa hivyo
kwa madai ya kukosekana kwa huduma bora, Serikali yake imeongeza vituo
vya afya kutoka 31 hadi 154, ingawa bado kuna changamoto ya wataalamu.
Dk
Shein aligusia suala la mrithi wake akisema yeyote atakayeonesha nia
kupitia CCM kwa wakati huu, atakuwa anakosea licha ya kwamba huu ndiyo
muhula wake wa mwisho.
“Hata kama namfahamu mtu ambaye naona anafaa, siwezi hata kumnong’oneza mpaka pale atakapopitishwa na chama,” alisema Dk Shein
chanzo;mpekuziblog.
Comments