Alisema wapo
baadhi yao, wamekuwa na mikoba miwili wanapokusanya mapato hayo na
kuyagawa kwa kuingiza kwenye mifuko ya makoti na mashati yao, na
nyengine ndio huziingiza serikalini.
Dk. Shein alitoa
angalizo hilo mjini Wete Mkoa wa kaskazini Pemba, mara baada ya
kulifungua soko na ofisi mpya ya baraza la mji wa Wete, ikiwa ni sehemu
ya shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar.
Aliwatahadharisha
wakusanya mapato hao kwa kuwambia “mti na macho’ akiwaashiria kuwa
suala la kukusanya mapato, hayataki ubabaisha uliokuwa umezoeleka hapo
awali.
Dk. Shein
alieleza kuwa, anazotaarifa rasmi juu ya wakusanya mapato katika mji wa
Wete, kuwa wapo baadhi yao ni wababaishaji, na kuwataka sasa waache
tabia hiyo mara moja.
Alisema sio vyema
mapato wanayoyakusanya kuyaingiza kwenye mifuko yao binafasi, na
mengine ndio kuyaingiza kwenye mfuko wa serikali, na sasa hatomvumilia
yeyote atakaebainika kuchupa taratibu zilizopo.
“Mnaokusanya
mapato kwenye mabaraza ya miji, halimashauri na taasisi nyengine, acheni
mtindo wa kuwa na mifuko miwili wakati mnapokusanya mapato, na badala
yake, eleweni kuwa fedha hizo hutakiwa kuingizwa serikali
pekee’’,alifafanua.
Katika hatua
nyengine Rais huyo wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapidnuzi,
alisema tayari serikali, imeshatenga shilingi milioni 600 kwa ajili ya
kuwafikisha huduma ya umeme wananchi wa Kisiwa cha Fundo wilaya ya Wete.
Alisema tayari
visiwa kadhaa vidogo vidogo vinavyoishi watu, vimeshafikishiwa umeme
kikiweo cha Mwambe shamiani, Kisiwa panza na Makoongwe, hivyo aliwata
wananchi hao wa kisiwa cha Fundo, kuondoa shaka.
Alifafanua kuwa
sasa kilichobakia ni mazungumzo ya mwisho na Shirika la Umeme la
Zanzibar ZECO, na anatarajia sana katikati ya mwaka huu, huduma hiyo iwe
imeshafika kisiwani humo.
Alisema miongoni
mwa azma na malengo ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964, ni
kuhakikisha wananchi wote wapata huduma za lazima bila ya ubaguzi.
Alisema waasisi
wa mapinduzi hayo, walishaamua kuwakomboa wananchi, ambao kwa muda mrefu
walikuwa wametawaliwa, na chama cha ASP ndio kilichowakomboa kwa wakati
huo.
“Sasa
tumeshajitawala wenyewe, hivyo hakuna sababu kwa wananchi wetu wa Fundo
wasipate huduma muhimu ya nishati ya umeme kama wenzao’’,alisema.
Hata hivyo rais
huyo wa Zanzibar, alisema malengo ya Mapinduzi matukufu, yameshafika
vilivyo Mkoa wa kaskazini Pemba, kwa kuwepo miundo mbinu ya barabara za
kiwango cha lami kila kijiji.
“Nani
engetarajiwa kuwa siku moja mkoa wa kaskazini Pemba, ungeng’ara kwa
barabara na huduma nyengine, kama za elimu, lakini haya yamekuja baada
ya sisi kjitawala na leo twasherehekea miaka 53 ya
Mapinduzi’’,alifafanua.
Katika hatua
nyengine rais huyo wa Zanzibar, aliitumia nafasi hiyo, kuwahakikisha
wananchi kuwa, wasiwe na wasiwasi wowote, hakuna uchaguzi mwengine hadi
mwaka 2020.
Alifafanua kuwa,
uchaguzi umeshakamilika na wala hakuna Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa
mwenye nguvu na mamlaka wa kuiondoa serikali ya Mapinduzi Zanzibar
iliochaguliwa kihalali.
“Sisi Zanzibar
tunakatiba yetu na sheria zetu, Umoja wa mataifa una taratibu zake na
sheria zake, sasa hakuna haki wala sheria kwa Umoja wa mataifa kuingilia
mambo ya ndani ya nchi yetu’’,alisema.
Akizungumzia
kuhusu soko hilo jipya, aliwataka wafanyabiashara, kuomba nafasi
zilizopo ili kulitumia kwa kutoa huduma kwa wananchi.
“Nimeelezwa kuwa
ndani ya soko hili jipya mna vikuta 78 na milango ya maduka kiasi 36,
sasa ombeni nafasi ili mfanyebiashara, muendeshe maisha
yenu’’,alifafanua.
Mapema Katibu
Mkuu wizara ya fedha na mipango Khamis Mussa Omar, alisema ujenzi wa
soko hilo jipya ni mradi maalum, ambo ni fedha za mkopo nafuu kutoka
benki ya dunia ‘W.B’.
Alisema mradi huo, upo wilaya zote nne za Pemba na manispaa ya zabnzibar, kwa
ujenzi wa masoko, ukuta, vidaraja vya kupitia wananchi, chinjio na
kulifanyia ukatabati mkubwa ofisi ya baraza la mji Mkoani Pemba.
Alisema ujenzi wa
soko hilo la Wete, pamoja na ofisi ya baraza la mji Wete, pia
umehusisha ujenzi wa maegesho ya gari, ambayo itakuwa na uwezo wa
kuchukua gari 30 za abiria kwa wakati mmoja.
Soko la matunda
na mboga mboga la Mjini Wete, limejengwa upya, baada ya lililokuwepo
lililojengwa mwaka 1954 kuchakaa, ambapo shilingi billion 1.73
zimetumika ikiwa ni mkopo wa masharti nafuu kutoka benki ya dunia (WB)
na sasa pana vyoo 14 vikiwemo vya watu wenye ulemavu.
chanzo: zanzibar24.
Comments