Dk. Shein atoa msamaha kwa wafungwa 14.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa maelekezo wakati alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika utekelezaji wa robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 01/11 /2016.RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ametoa msamaha kwa Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo 14 ikiwa ni miongoni mwa sherehe za kutimiza miaka 53 ya Mapinduzi matukufu ya Januari 12, 1964.

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa kisheria chini ya kifungu namba 59 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Dk. Shein ametoa msamaha huo kwa Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo  14.

Msamaha huo ambao hutolewa kila mwaka katika kipindi cha sherehe za Mapinduzi matukufu, huwahusisha wafungwa ambao ni wazee sana, wenye maradhi sugu au wenye makosa madogo ambao wamebakisha muda mdogo wa kutumikia chuoni, kuonesha nidhamu nzuri chuoni na kujutia makosa yao.

Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo, wenye makosa kama vile kuua kwa makusudi, wizi wa kutumia nguvu, wizi wa mali ya serikali, makosa ya kudhalilisha wanawake na watoto, makosa ya dawa za kulevya na wenye makosa mengi ya zamani kwa kawaida huwa hawapewi msamaha.

chanzo; zanzibar24.

Comments