Gazeti hili limebaini hayo katika uchunguzi wake maeneo mbalimbali
pamoja na kwenye masoko wilayani hapa. Bei hiyo imependa kuanzia Agosti
na Septemba mwaka jana na haijashuka hadi sasa.
Baadhi ya wafanyabiashara wa nafaka kwenye soko kuu la mjini Bunda,
katika jimbo la Bunda mjini na kwenye soko la mji mdogo wa Kibara,
katika jimbo la Mwibara, walisema kwa nyakati tofauti kuwa, bei ya
chakula imepanda kutokana na kuwepo upungufu mkubwa wa chakula katika
maeneo hayo.
Walisema kuwa hali hiyo imetokana na mvua kutokunesha wilayani hapa
kwa kipindi kirefu na kusababisha mazao yaliyokuwa yamelimwa mashambani
kukauka na pia wakulima wengine kushindwa kulima kwa sababu yakuwepo
ukame huo.
Walisema kuwa wamekuwa wakiuza chakula hicho wanachokipata kutoka
katika mikoa jirani kwa bei kubwa na kwamba wao pia ulazimika kukiuza
kwa bei hiyo ili waweze kurudisha mtaji wao pamoja na faida kidogo tu.
Mfanyabiashara katika soko kuu la Bunda, Esta Samson, alisema kuwa
kwa ujumla hali ya chakula katika wilaya inahitaji tahadhari na kwamba
hata biashara yao haiendi kama iwalivyokuwa wanatarajia.
“Hali ya chakula katika hili soko letu ni mbaya maana kimepanda sana
kutokana na sisi tunavyouziwa kwa bei ya juu sana. Na hii hali tuseme
imeaanza mwezi wa nane na wa tisa mwaka jana. Sasa hivi gunia moja la
mahindi tunalinunua kati ya sh 110,000 hadi sh 120,000,” alisema Samson.
Baadhi ya wananchi walisema kuwa wanakabiliwa na njaa kubwa na kwamba
hali hiyo inatokana na ukame na pia baadhi ya mazao yao yaliyokuwa
shambani yalishambuliwa na wanyama, wakiwemo tembo kutoka katika Hifadhi
ya Taifa ya Serengeti.
chanzo:habarileo.
Comments