Ushahidi
katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi inayomkabili,
Salum Njwete (34) maarufu Scorpion, umeshindwa kuendelea baada ya
upande wa Jamhuri kudai shahidi hakufika.
Sababu
za kutofika kwa shahidi huyo ambaye ni daktari kutoka Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH) ni kutokana na kuwa nje ya kituo chake cha kazi
hivyo hakupatikana jana.
Mshitakiwa
Scorpion alipandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Wilaya ya
Ilala, mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule, wakati shauri hilo
lilipopelekwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi upande wa Jamhuri.
Wakili
Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga, alidai upande wa Jamhuri
ulipanga kumhoji shahidi ambaye ni daktari lakini kwa vile alikuwa na
dharura ingefaa mahakama impangie tarehe nyingine.
“Mheshimiwa
hakimu shauri lilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na upande wa Jamhuri
ulipanga kumleta shahidi ambaye ni daktari lakini ameshindwa kufika leo,
ana dharura ambayo inaweza ikachukua wiki tatu.
“Hivyo
kwa mujibu wa kifungu namba 225 cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi ya
Makosa ya Jinai ambayo inataka kesi isiahirishwe zaidi ya wiki mbili
kama mshitakiwa yuko mahabusu, tunaomba mahakama itaje hapa tupange
tarehe ya kusikilizwa,’’alisema.
chanzo;mpekuziblog.
Comments